TANGAZO
WALIMU katika shule ya msingi Nambaza Kata ya Nansimo wilayani Bunda, wamesema watahama shule hiyo endapo serikali ya wilaya hiyo haitachukua hatua madhubuti kukomesha ushirikina shuleni hapo.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Sospiter Mafuru, alisema walimu wake wanafanyiwa vitendo vya ushirikina ikiwa ni pamoja na kusumbuliwa usiku na kunyolewa nywele sehemu za siri.
Alitaja vitendo vingine kuwa ni kuvuruga vyombo vya ndani wakati wa usiku, kumwaga michuzi na damu kwenye mashuka na nguo za walimu hao

“ Vitendo hivi vimetishia usalama wa walimu hadi sasa walimu watatu wa kike wamehama shule hii kwa hiyo tunaomba jamii ya Nambaza wachukue hatua,”alisema.
Alisema awali ushirikiana huo ulianza kwa wanafunzi kuugua na kuanguka ovyo na baadaye kwa walimu na aliomba Serikali kuchukua hatua na kukaa na wananchi wao.
Mafuru alisema hadi sasa ana walimu tisa,wa kike watano na wa kiume wanne.
Mkuu wa wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe, alisema tayari ameviagiza vyombo vya dola kwenda kijijini hapo kufanya utafiti kuwabaini watuhumiwa hao.

Facebook Blogger Plugin by Harocq
Post a Comment