TANGAZO
Chris Brown aliingizwa chaka na marafiki zake waliomwambia kuwa Karrueche Tran alikuwa na hamu kubwa ya kurudiana naye – hali ambayo ilisababisha seke seke kwenye club ya usiku waliyokutana na kumfanya Chris aonekane kama mtu anayelilia penzi la Karrueche, TMZ wameripoti.

Vyanzo vilivyo karibu na wapenzi hao wa zamani vimeiambia TMZ kuwa Chris alichukua meza kwenye club ya Playhouse, iliyokuwa karibu na meza ya Karrueche kwasababu marafiki zao walimwambia afanye hivyo.

Marafiki hao walikuwa wakimjaza Chris kuwa KT yupo tayari kuyamaliza.

Hata hivyo Chris alibaki na butwaa baada ya kumshuhudia Karrueche akiondoka kwenye club hiyo kwa hasira utadhani aliona jini.

Kuna kila dalili kuwa Chris na Karrueche hawatarudiana tena!

                                         Angalia Video Hapa chini:

                            

Je wewe unakabiliwa na changamoto ya kipato kama nilivyo nayo mimi??..basi kama ndiyo njoo nikuonyesha njia ya kukuza kipato hicho pamoja na kutekeleza malengo yako...nipigie 0784 778788

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by Harocq

Post a Comment



 
Top