Mpenzi msomaji wiki iliyopita nilidokeza kuwa katika simulizi hii nitahakikisha najibu maswali yote ambayo yamekuwa yakiulizwa sana na wasomaji.
SASA ENDELEA…
Je, mtu anawezaje kujiunga nao na kwamba kuna ukweli kuwa atapata utajiri kwa kufumba na kufumbua macho? Je, ni masharti au vigezo gani ambavyo lazima uvitimize ndiyo ujiunge nao? Fomu za kujiunga zinapatikanaje na wapi? Je, wana makao yao hapa nchini au Afrika Mashariki?
Je, ni kweli wanaamini Yesu na Lucifer (shetani mkuu) ni mtu na ndugu yake? Je, ni kweli wanatumia Biblia na wanapomzungumzia ‘Bwana’ huwa hawamaanishi Yesu bali Lucifer ambaye ndiye wanayemwabudu?
Je, ni kweli kwamba ni watu wenye nguvu mno na mambo yao ni makubwa mno na siri zao ni nzito mno hapa duniani?
Je, kuna makundi mangapi ya Freemasons? Je, ni kweli wapo Freemasons wa kale na wa sasa? Utofauti wao ni nini?
Je, ni kweli kwamba ili uwe Freemason kuna ngazi au shahada ambazo lazima mtu upitie ili ukamilike? Ni viongozi gani wakubwa duniani ni wanachama? Je, ni wasanii gani duniani wamejiunga Freemasonry?
HISTORIA YA FREEMASONS
Ukitaka kukijua kitu vizuri ni vyema ukawa na kasumba ya kujua historia yake. Siwezi kuyajibu maswali hayo bila kujua mzizi wa Freemasons.
Vitabu vikubwa nilivyosoma vinaturudisha nyuma hadi miaka 1700 baada ya Kristo.
Freemasonry ni jumuiya ya kale mno lakini ilianza kabla ya 1717. Kabla ya hapo haikufahamika rasmi.
Kama nilivyotangulia kusema toleo lililopita. Freemasonry walikuwa ni waashi ambao walikuwa na utaratibu wao wa namna ya kufanya ujenzi wao.
Freemasons walikuwa ni mafundi ujenzi waliokuwa huru kwa namna ya ujenzi wao. Hawa waashi au mafundi walijikita katika Ulaya ya zama za kati wakiruhusiwa kuzunguka kila mahali kote duniani kama wangeweza.
Awali, hawakuwa watu ambao walikuwa wakijihusisha na mambo ya maajabu kama wanavyodaiwa kufanya Freemasons wa sasa. Watu hawa walianza kuhusishwa na mafundisho ya kipagani na uchawi kutoka Mashariki ya Kati na huko Asia Magharibi.
Freemasons hao ambao walikuwa wajenzi wa zama za kati za Ulaya walifahamika kwa jina la kazi yao, yaani mason au kwa lugha yetu fundi mwashi. Masoni kama nilivyotoholewa kwenye Lugha ya Kiingereza, walikuwa na utaratibu maalum wa kulinda siri zao zinazoendana na kazi yao.
Freemasons walianza kwa kujenga mahekalu yao. Ndani yake wanajumuiya walifundishana maajabu na siri za kazi zao za ujenzi. Lakini haya hayakufafanuliwa kwa mtu asiyejua kilichokuwa kikiendelea.Hivyo kilichotokea ni kwamba kuliibuka majengo mbalimbali ya ibada zama hizo, majengo ya kiserikali, makasiri ya kifalme na nyumba za watu binafsi wenye ushawishi wa kiuchumi katika jamii.
Kwa kuwa elimu hiyo haikutolewa kwa kila mtu ndiyo maana Ulaya ya zama hizo haikunufaika na maarifa haya. Elimu hiyo ilikuwa ni kwa watu maalum na walitumia kwa majengo ya watu na vikundi mahususi tu.
Siku zote Freemasons walichonacho ni cha kwao na ulichonacho pia wanataka wakichukue, daima wako kinyume na jamii inayowazunguka, hivyo lolote la kuinufaisha jamii halielezwi kwa wanajamii na wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wanajamii hawayapati maarifa hayo.
Desturi hii Freemasons wako nayo hadi leo hii. Kuna madai kwamba kila shida unayoiona duniani au maradhi ujue kuna tiba yake, kuna tiba ya kansa, kuna tiba ya Ukimwi, kuna suluhisho juu ya tatizo la uchumi, kuna suluhisho juu mmomonyoko wa maadili lakini katu hayatatolewa, kwa sababu wewe unayesoma hapa ndiye adui yao nambari moja!
Freemasons wa zama za kati katika mahekalu yao walihifadhi zana zao za kazi, walipumzika humo na pia kula chakula humo.
Katika mahekalu hayo wanajumuiya walisimikwa katika madaraja ya kimasoni, zama hizo kulikuwa na madaraja matatu tu, yaani Apprentices (wanafunzi wa mwanzo), Journeymen (wanafunzi wa kati kuelekea kuiva) na Grandmaster (waliofuzu).
Kwa nini ilibidi kusubiri kwa takriban miaka sabini kupata fursa ambayo kwayo Freemasonry ya leo imezaliwa?
Usikose kila Jumatano katika gazeti hili la Risasi Mchanganyiko.